(Paul Gasol akiwamchezoni kwenye NBA.)
Gasol ambaye aliwahi pia kuvichezea vilabu vya Memphis Glizzlies, Chicago Bulls, San Antonio Spurs na Milwaukee Bucks na hatimaye kurudi Barcelona mwaka 2021amesema kuwa, ameseama haikuwa rahisi kuchukua uamuzi huo lakini hakuwa na namna yoyote.
“Ninastaafu kucheza kikapu. Ni uamuzi mgumu baada ya kucheza kwa miaka mingi, lakini ni uamuzi ambao nimeshauchukua”. Alisema Mkali huyo wa kushambulia kwa mabavu.
Baada ya kauli ya Gasol kustaafu, Nae mkurugenzi wa NBA, Adam Silver amemshukuru sana na kumwagia sifa Gasol kwa kuwahamisha mashabiki, kuwa mtu wa kujitolea kwenye jamii na kuwa balozi mzuri wa NBA.
“Haina mashaka Paul Gasol ni moja ya wachezaji waliokamilika kwenye kizazi chake. Ubingwa wa NBA mara mbili, kucheza timu ya Nyota wa NBA ‘NBA All-Stars’ mara sita, kutwaa medali moja ya ubingwa wa Olympic na mbili za Ulaya”.
“Paul aliwahamasisha mashabiki wengi kipindi cha ubora wake, Lakini kitu kinachomfanya aendelee kuwa wakipekee, ni zile juhudi zake za bila kuchoka zakurudishakwa jamii za Hispania na kwenginekoDuniani” Amesema Silver.
NBA wakamaliza kwa kumpongeza “Tunampongeza sana Paul kwa kuwa balozi mzuri wa NBA”.
Kwa upande mwingine, klabu yake aliyocheza kwa mafanikio sana, Lakers ambayo alibeba nayo ubingwa wa NBA mwaka 2009&10 inaelezwa ipo kwenye mpango wa kuistaafisha jezi yake ya namba16 ikiw ani heshima ya kuthamini mchango wake uliotukuka klabuni hapo.
Gasol amestaafu baada ya kucheza NBA kwa takribani miaka 20 akiwa na wastani wa kupata alama 17 na rebound 10 kwenye michezo 1226 aliyocheza.





