Kushoto ni Halfan Athumani wakati akizimba bomba, na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph, akimkabidhi zawadi
Halfan Athuman alionekana katika mtandao wa kijamii wa Instagram kwenye ukurasa rasmi wa Mamlaka ya Majisafi na Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) akifanya kazi ya kuziba bomba kubwa la inchi 16 liliokuwa limepasuka eneo la Chinangali Park jijini Dodoma.
Kwa upande wake Waziri Aweso alipokutana na Halfan kwa mara ya kwanza alimuagiza Mkurugenzi wa DUWASA kumtambulisha kwa bodi ya mamlaka hiyo ili awe katika mipango ya kupewa fursa zaidi katika ngazi yake ya kazi.





