Thursday , 7th Oct , 2021

Kocha wa Taifa Stars, Mdenmark Kim Poulsen amesema ana imanikubwa kikosi chake kitaibuka na ushindi kwenye mchezo wake wa mzunguko watatu wa kundi J kuwania kufuzu kombe la Dunia leo Oktoba 7, 2021 kwenye dimba la Mkapa.

(Kikosi cha Taifa Stars kilichocheza dhidi ya Madagascar mwezi uliopita na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 kwenye dimba la Mkapa)

Kim Poulsen amesema, “Tumeingia kambini siku chache zilizopita ila tunafanya mazoezi mazuri, tuna matarajio makubwa ya kushinda mchezo huu, haya ndiyo malengo yetu makubwa na hata Watanzania wote kwa ujumla”.

Kwa upande wa wachezaji, mshambuliajiJohn Rafel Bocco amesema wamejipanga kupanda ushindi kwenye michezo yote hususani kwenye dimba la nyumbani ili kufuzu kombe la Dunia mwakani.

"Tunatammbua mechi itakuwa mgumu kwa kuwa hata wenzetu wejipanga, lakini màlengo yetu ni kuhakikisha tunashinda mechi zotee nyumbani ili kupambana na hatimaye kufuzu kombe la Dunia mwakani” Amesema Bocco.

Kwa upande wa hali ya wachezaji, Stars imewajumuisha kikosini, John Rafael Bocco na Kibu Denis waliokosekna kwenye mchezo dhidi ya Madagascar wakati walizni Erasto Nyoni na Bakari Mwamnyeto wakiwa na majeraha ilhali  walinzi Kennedy Juma na Dickson Job wapo fiti.

Stars ndiye kinara wa kundi akiwa na alama 4 akifuatiwa na Benin mwenye alama 4 pia ila Stars akiwa anaongoza wa utofauti wa magoli ya kufunga kwani amefunga mabao 4 na kufungwa 3 wakati ambao Benini amefunga 3 na kufungwa mabao 2.

Wawili hao wanatazamiwa kucheza tena siku tano baadaye huku Benini akitazamiwa kuwa mwenyeji wa mchezo huo.