Monday , 11th Oct , 2021

Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufikisha mabao 80 kwa upande wa timu za taifa za bara la Amerika kusini na kumpiku gwiji wa Brazil, Pele mwenye(77).

(Lionel Messi akikabidhiwa picha zawadi ya heshima yenye picha yake na muwakilishi kutoka shirikisho la soka Argentina ikimuonesha akiwa amebeba kombe la Copa Amerika walilolitwaa mwaka huu na yeye akitoa mchango mkubwa pamoja na kuwa mchezaji bora wa mashindano)

Messi ameweka rekodi hiyo usiku wa kuamkia leo baada ya kufunga bao la kwanza kabla ya Rodrigo De Pol na Lautaro Martinez kufunga bao la pili na la tatu kwenye ushindi wa 3-0 wa Argentina dhidi ya Uruguay kufuzu WC 2022.

Baada ya kufunga bao hilo la kihistoria, Messi ameongelea mchezo huo namna ulivyokuwa kwa kusema,

“Tulicheza mchezo mzuri sana. Kila kitu kilienda kwa usahihi mkubwa. Uruguay wanakusubiria na wanatengeneza hatari. Pindi tulivyopaya goli la kwanza, tulianza kupata nafasi na magoli yakatoke” Alisema Messi.

Argentina ipo nafasi ya pili kwenye kundi la kuwania kufuzu barani Amerika Kusini ikiwa na alama 22 ilhali vinara Brazil ina alama 28 baada ya wawili hao kucheza michezo 10  wakati Ecuardo na Uruguay watatu na wanne wakiwa na alama 16