Friday , 15th Oct , 2021

Polisi nchini Kenya wamefanikiwa kumkamata Emmanuel Ritoch ambaye anayetuhumiwa kwa kesi ya mauaji ya mke wake ambaye alikuwa mwanariadha wa kimataifa nchini Kenya, Agnes Tirop kilichotokea Jumatano Oktoba 13, 2021.

Askari Mkuu wa kituo chas Polisi Changamwe, Tom Makori amethibitiha kukamatwa na kusekwa rumande kwa Emmanuel amliyekamatwa pwani ya Mombasa akijaribu kutokroka nchini Kenya.

Askari huyo amesema, “Mtuhumiwa amekamatwa leo na yupo rumande kwenye kituo cha Polisi cha Changamwe. Ninathibitisha kuwa tunamshikilia mtuhumiwa wetu na yupo ruamande” Amesema Makori.

Nae Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, George Kinoto amesema mtuhumiwa atafanyiwa mahojiano na kukutwa na mkono wa Sheria endapo akikutwa hatiani kwa kosa la mauaji ya mke wake Agnes Tirop aliyeacha simanzi kubwa.

Ikumbukwe kuwa, Askari Mkuu wa kituo cha Polisi Changamwe, Tom Makori alithibitisha kuwa siku ya Jumatano Oktoba 13, 2021 Agnes Tirop alikutwa amefariki nyumbani kwake maeneo ya Iten.

Polisi wakaendelea kwa kusema mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa umetoka damu nyingi na kuonekana umechomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na tumboni jambo ambalo linaaminika limechukua uhai wa Mwanariadha huyo.

Tirop alishika nafasi ya pili  mara mbili kwenye mashindano ya riadha ya Dunia na kushinda medali ya shaba mwaka 2017 na 2019 pamoja, kushika nafasi ya nne kwenye mbio za mita 5,000 Tokyo Olympic mwezi Agosti 2021 na kuweka rekodi ya Dunia ya kushiriki mbio za mita 10,000 nchini Ujerumani.