Saturday , 16th Oct , 2021

Klabu ya Barcelona imesema haina mpango wa kumrejesha mlinzi wake wa zamani Dani Alves ambaye kwasasa ni mchezaji huru.

Dani Alves

Beki huyo wa Brazil, mwenye umri wa miaka 38 ambaye aliondoka Barcelona miaka mitano iliyopita, amesema yupo tayari kurejea Nou Camp kwa mshahara unaoendana na klabu hiyo inayopitia kipindi kigumu kiuchumi na kimatokeo.

Barcelona ambayo haipati matokeo mazuri kwa siku za karibuni, ingeweza kuinasa saini ya Alves ambaye hana timu baada ya kuachana na Sao Paulo majuma kadhaa yaliyopita kwa madai ya kutokulipwa mshahara kwa muda mrefu.

Beki huyo wa zamani wa Sevilla, aliondoka Barcelona katika msimu wa 2015/2016, akishinda La Liga na Copa Del Rey kwenye msimu wake wa mwisho ambapo baadaye alitimka Juventus, na PSG alikocheza kwa mafanikio.