Monday , 18th Oct , 2021

Kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema kuwa kwa mwenendo wa mshambuliaji wa klabu hiyo na timu ya Taifa ya Ufaransa Karim Benzema, anastahili kushinda Balon D’or mwaka huu.

Picha ya Kocha Zidane na Benzema

Zizou amesema "Karim ni mchezaji mzuri, anajua kufanya kila kitu uwanjani ninatumahi atapewa tuzo hii ya Ballon d'Or".

Benzema yupo kwenye shortlist ya wachezaji 30 wanaowania tuzo hiyo mwaka huu akiwa na Ronaldo, Messi, Kante, Lewandowski, Salah, Mbappe, Neymar na wengine wengi