Tuesday , 19th Oct , 2021

Kufuatia tuhuma zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mipasuko iliyo katikakati ya barabara ya kuruka na kutua ndege kwenye uwanja wa ndege wa Chato uliopo mkoani Geita, taarifa hizo hazina ukweli wowote na wananchi wameombwa kuzipuuza kwani uwanja huo bado mpya na unatumika.

Sehemu ya uwanja wa ndege wa Chato

Hayo yamesemwa na Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mhandisi Haroun Senkuku, wakati anakagua na kutolea ufafanuzi juu ya skendo iliyohusisha uwanja huo kuwa na mipasuko mikubwa iliyoota nyasi.

Aidha Mhandisi Senkuku amesema serikali imetumia zaidi ya shilingi bilioni 58 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja huo unaojengwa kwa awamu ambao una urefu wa kilomita tatu na upana mita 45 ambao bado upo kwenye hatua za ukamilishaji.