Wednesday , 20th Oct , 2021

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Neema Lugangira amesema ni wakati sasa wa taifa kupitia Tume ya Tehama kufikiria kuanzisha kodi za kidijitali ikiwa ni sehemu ya hatua kuelekea ujenzi wa taifa na uchumi wa kidijitali.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Neema Lugangira

Lugangira ameyasema hayo leo Oktoba 20, 2021, wakati akichangia hoja kwenye kongamano la Tehema lililofanyika kwenye ukumbi wa Simba ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

''Wanawake kwenye siasa wanapitia changamoto sana mitandaoni, naongea hili mimi kama mbunge ambaye nakumbana na hilo na iko wazi kuna chuki kubwa na ubaguzi nadhani tunatakiwa kuangalia sera ya ICT inasemaje ili kusaidia kundi hili na pengine uwepo wa kodi za kidijitali utasaidia kudhibiti hili,'' ameeleza Neema Lugangira.

Amesisitiza kuwa dunia kwasasa inabadilika hivyo ni vyema kwenda sawa na mataifa mengine duniani yanavyofanya hususani kwenye makampuni makubwa ya Tehema yenye usajili ndani na nje ya nchi zao kama Google na mengine ambayo hulipa kodi kutokana na makubaliano ya usajili wao.

Hata hivyo Mkurugenzi Mkuu wa Tehama Samson Mwela amesema wameuichukua ushauri huo na wataitisha mkutano wa wadau ili kuona jinsi gani watatekeleza.

Samson Mwela (kushoto) Mkurugenzi Mkuu Tume ya TEHAMA

''Tunaompango mkubwa wa kuwasaidia Start ups kwenye TEHEMA lakini pia tutakaa na washirika/wadau mbalimbali nadhani mwezi Novemba, ili kuona jinsi gani wanafikia lengo lakini pia hata haya masuala ya kodi kidijitali tutajadili kwa pamoja,'' ameeleza Samson Mwela, Mkurugenzi Mkuu Tume ya TEHAMA.