Thursday , 21st Oct , 2021

Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Simiyu, kimewataka viongozi wa chama hicho na serikali wilaya ya Busega, mkoani humo, kuhakikisha kiasi cha shilingi bilioni 1.8 walizopewa na Mhe Rais Samia zinatumika ipasavyo kujenga miradi na si vinginevyo.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohamed Seif

Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohamed Seif, kwenye kikao cha wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho wilayani Busega, katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero ngazi ya mashinani.

Kufuatia maagizo hayo, Mkuu wa wilaya ya Busega, Gabriel Zakaria, amesema fedha hizo zitatumika kama ilivyopangwa kujenga vyumba vya madarasa.