Monday , 25th Oct , 2021

Motorola wapo katika majaribio ya Teknolojia mpya ya “Space Charging” kifaa ambacho kinaweza kuchaji simu nne kwa wakati mmoja hata ukiwa umbali wa mita tatu.

Picha ikionesha namna Teknolojia ya “Space Charging” inavyofanya kazi

Kifaa hicho kinatumika kuchaji simu kama unavyotumia Internet au Bluetooth, hakuna ulazima wa kuchomeka waya wa kuchajia au kuiweka katika wireless charge ya karibu na endapo itathibitika kuwa hakuna madhara kiafya kwa sababu umeme unaopita hewani baada ya kukaguliwa basi mfumo huu utaanza kutumika rasmi.