Wednesday , 27th Oct , 2021

Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera linamshikilia Emmanuel Zakaria (38) mkazi wa Lusahunga wilayani Biharamulo kwa tuhuma za kumkuta akishiriki mapenzi na Mbuzi katika kichaka.

Mbuzi

Kamanda wa polisi mkoani Kagera Awadhi Haji, amesema kuwa baba huyo alikutwa na mpita njia akifanya kitendo hicho Oktoba 24 mwaka huu saa 09:00 Alasiri, ambaye alipiga kelele zilizosababisha wananchi kufika haraka na kumkamata.

"Wananchi walimkuta akiwa uchi akimfanyia Mbuzi kitendo hicho, walimkamata na kumkabidhi polisi, tunaye na tunaendelea kumhoji, lakini pia atapimwa afya ya akili ili kubaini kama hana tatizo ya ugonjwa wa akili na baadae hatua za kisheria zitafuta" amesema Kamanda Awadhi