Kamanda wa Jeshi la Zimamoto mkoani Mwanza,Ambwene Mwakibete
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Jeshi la Zimamoto mkoani Mwanza Ambwene Mwakibete, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini humo, na kusema jeshi hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi bado wanaendelea na uchunguzi zaidi ili kuweza kuwabaini waliofanya njama hizo za kuteketeza baa hiyo
Aidha Mwakibete amekanusha kuwepo kwa taarifa za upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii zinazosema gari la zimamoto lilifika katika eneo la tukio bila kuwa na maji.






