Thursday , 28th Oct , 2021

Benki Kuu ya Tanzania imetoa onyo na kusema kwamba itawachukulia hatua watu wote wanaotunza kwenye sherehe kwa mtindo wa kurusha fedha na kuanguka sakafuni, kuzikunjakunja na wakati mwingine kuzitumia kama mapambo kwani kufanya hivyo ni kuitweza fedha.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga

Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 28, 2021, na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga, na kusema kwamba fedha hizo wakati mwingine huwekwa kwenye mwili wa mtu aliyeloa jasho na kusema vitendo hivyo vinasababisha fedha hizo kuchakaa na kuiongezea serikali gharama kubwa ya kuchapisha noti mpya.

Mbali na hayo Benki Kuu imewashauri washiriki katika matukio yote ambayo yanahusisha matukio ya fedha, kuandaa vyombo maalum vya kuwekea fedha hizo badala ya kufanya vitendo ambavyo havikubaliki.

Hivi karibu Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, alitoa onyo kuhusu watu wanaotunza fedha kwa kuzitupa chini kwani ni kinyume cha sheria.