
Dean Smith.
Makocha wengine ambao walipoteza ajira zao ni Xisco Munoz wa Watford, Steve Bruce wa Newcastle United, Nuno Espirito Santos wa Tottenham na Daniel Farke wa Norwich City.
Dean anaondoka baada ya Ijumaa iliyopita kukiongoza kikosi cha Villa na kukutana na kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Southampton katika dimba la St Mary's.
Aliyevuruga mipango yote katika mchezo huo wa tano mfululizo kupoteza msimu huu ni Adam Armstrong ambaye aliwapa ushindi waajiri wake Southampton ndani ya dakika za mwanzo za mchezo huo kipindi cha kwanza.
Matokeo ambayo yalimlazimisha Mkurugenzi wa Aston Villa, Christian Purslow kudai wazi kuwa “Msimu huu hatujaona maendeleo katika kikosi chetu, kiwango na nafasi tuliyopo hailingani na malengo yetu, tumeamua kufanya mabadiliko mapema kumpa nafasi kocha mpya kuja na kuonyesha maendeleo katika kikosi chetu,”amesema.
Dean Smith alitajwa kuwa kocha wa Villa Oktoba 2018 ambapo alikiongoza kikosi hicho kupanda daraja katika msimu wake wa kwanza, lakini kwa sasa imeonekana mambo hayapo sawa.