
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai
Spika Ndugai ameyasema hayo Jijini Dodoma kwenye mafunzo ya uongozi kwa wanawake viongozi na wanasiasa ambapo amesema kama kundi la wanawake wakipewa mamlaka halafu wakaanza kuvimba na kushurutisha wengine kwa kuwaweka watu ndani basi ni wazi kunawaondolea sifa ya kuwa viongozi.
Kwa upande wake Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema wao wakiwa ni miongoni mwa wanawake wachache waliobahatika kupata nafasi za juu za uongozi wanahakikisha kufanya vizuri zaidi ili kubadili fikra mbaya za baadhi ya watu kuhusu wanawake viongozi.