
(Kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane)
Solskjear alifukuzwa baada ya United kufungwa 4-1 na Watford katika dimba la Vicarage road hii ikiambatana na rekodi ya Manchester kushinda mechi moja pekee katika michezo saba iliyopita katika mashindano yote.
Taarifa kutoka kwenye chanzo cha karibu na Zizzou zinasema kuwa Mfaransa huyo anatazamia kuchukua nafasi ya kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Ufaransa au PSG iwapo nafasi itajitokeza.
Zidane alishinda mataji matatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa kwanzia mwaka 2016 na baadaye kuondoka 2018 na kurudi mwaka mmoja baadaye ambapo alitwaa kombe la La Liga na Kombe la Hispania, na baadaye mwezi mei mwaka huu aliamua kuachana na Galacticos.
Mauricio Pochettino, ambaye anatajwa kuwa kocha wa Manchester United kwenye siku za usoni ndiye kocha wa PSG kwa sasa na yupo katika nafasi nzuri ya kuwa kocha wa Manchester ingawa Mashetani wekundu bado awajaanza mazungumzo naye.