
(Mkurugenzi wa Michezo, Yussuph Singo (katikati) akiongelea maandalizi)
Kuelekea kwenye mchezo huo, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yussuph Singo amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika huku wageni Uganda wakitaraji kuwasili nchini leo Disemba 7,2021.
"Mpaka sasa maandalizi yamekamilika na wachezaji wapo vizuri kwa ajili ya mechi hiyo ya kirafiki ambayo lengo kubwa ni kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania inayofanyika kila mwaka" amesema Singo.
Katika maadhimisho hayo pia kutakuwa na mchezo wa soka wa wanawake ambapo Timu ya Taifa ya Uganda ya Wanawake na timu ya Taifa ya Tanzania ya wanawake ‘Tanzanite’ watakaoshuka dimbani saa 11:00 usiku.
Kwa upande wa Viingilio, Mkurugenzi Singo amesema, viingilio ni Sh. 2000 mzunguko huku VIP A na VIP B ni Sh. 5,000 lengo la kuweka viingilio hivyo ni ili kila mwananchi aweze kushiriki na kufurahia maadhimisho hayo.
"Tumeweka viingilio rafiki ili kila mtanzania aweze kushiriki tufurahie maadhimisho kwa pamoja," alisema Singo.
Wachezaji wa Taifa Stars ni Metacha Mnata (Polisi Tanzania), Haroun Mandanda (Mbeya City), Musa Mbisa (Coastal Union), Nathaniel Chilambo (Ruvu Shooting), Kelvin Kijiri (KMC), Hans Masoud (Coastal Union), Nickson Kibabage (KMC) na Oscar Masai (Geita Gold).
Wengine ni Abdulrazack Mohamed (KMC), Lusajo Mwaikenda (Azam), Abdulmajid Mangalo (Biashara United), Nashon Naftari (Geita Gold), Tariq Simba (Polisi Tanzania), Sospeter Bajana (Azam), Hassan Nassor (Dodoma Jiji) na Abdul Hamis Suleiman (Coastal Union).
Pia wapo Meshack Abraham (Kagera Sugar), Cleophace Mkandala (Dodoma Jiji), Denis Nkane (Biashara United), Rashid Juma (Ruvu Shooting), Vitalis Mayanga (Polisi Tanzania), Anuary Jabir (Dodoma Jiji).