
(Max Verstappen (ushoto)na Lewis Hamilton (kulia).
Suala la rufaa limekuja baada ya malalamiko ya awali ya kambi hiyo kutupiliwa mbali na shirikisho la mbio za magari Formula 1 muda mchache baada ya mchezo huo kumalizika Abu Dhabi.
Malalamiko ya kambi ya Hamilton yanaeleza kuwa, msimamizi wa mchezo aliruhusu kinyume na utaratibu magari kupitana wakati gari la ukaguzi wa usalama lilikuwa lilipokuwa lina malizikia kukagua ajali ya Nicholas Latifi.
Pia wamesisitiza kuwa, Msimamizi wa mashindano hayo, Michael Masi hakuwatafsiri sheria vizuri kwani kabla ya kuanzisha mzunguko mwingine hakumkagua Verstappen ambaye alikuwa anasimama karibu na Hamilton.
Kambi ya Hamilton inaamini sababu hizo mbili ndizo zilizoamua mazingira ya Verstappen kuwa bingwa kwenye mzunguko wa mwisho licha ya kuaongozwa kwenye mizunguko iliyopita.
Kama Hamilton angefanikiwa kuibuka na ubingwa wa Abu Dhabi Grand Prix, basi angeandika rekodi mpya ya kuwa dereva pekee kuwahi kushinda ubingwa wa dunia wa Formula 1 mara 8 na kumpiku Schumaker mwenye 7.