Friday , 24th Dec , 2021

Gwiji wa soka Nchini Brazil, Edson Arantes Do Nascimento ‘Pelle’ (81), usiku wa kuamkia leo ameruhusiwa kutoka hospitali na kurudi nyumbani kwake baada ya afya yake kuimaraika.

(Gwiji wa Soka Nchini Brazil, Pelle)

Hospitali ya Albert Einsten iliyopo Sao Paulo nchini humo, imeeleza kuwa hali ya kiafya ya nyota huyo inaendelea vizuri ndiyo maana ameruhusiwa kwenda nyumbani lakini akiwa bado kwenye dozi ya matibabu yake.

Baada ya kuruhusiwa kwenda nyumbani, Pelle akaandika kwenye akaunti za mitandao yake ya kijamii kuwa “Kama nilivyo waahidi, nitasheherekea Christmas na familia yangu. Nipo njiani kuelekea nyumbani. Ahsanteni wote kwa jumbe nzuri”.

Ikumbukwe kuwa, Pelle alilazwa hospitalini hapo tokea Disemba 9, 2021 kwa ajili ya kupata tiba maalum ya Saratani ya Utumbo iliyogundulika Septemba 9 mwaka huu na kupata tiba ya ‘Chemotheraphy’ baada ya kuzidiwa.