
Jack Grealish
Jack Grealish mwenye umri wa miaka 26 ndio mchezaji wa England mwenye thamani kubwa zaidi, aliweka rekodi hiyo baada ya kununuliwa na Manchester City akitokea Astoni Villa kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 100 ambayo ni zaidi ya bilioni 308 kwa pesa za kitanzania.
Grealish amezungumzia maisha yake ndani ya Manchester City tangu alipojiunga na mabingwa hao wa England na kuweka wazi kuwa mambo ni magumu tofauti na alivyotarajia,
"Nimefanya vizuri hadi sasa, nina mengi zaidi ya kufanya. Imekuwa ngumu zaidi kuliko vile nilivyofikiria itakuwa, bado ninajifunza na kuzoea nimesikia watu wengine wanachukua mwaka kuzoea hapa, labda itakuwa hivyo kwangu’’.
Kiungo huyo tayari ameshaitumikia Manchester City kwenye michezo 15 kwenye michuano yote na amefunga mabao 2 lakini pia kapiga pasi za usaidizi wa magoli (assist) 3.