Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee
Kauli hiyo ameitoa Bungeni jijini Dodoma hii leo Februari 4, 2022, ambapo Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, alimuahidi kufuatilia na kumpa jibu kinachopelekea barabara hiyo kutokamilika hadi sasa.
"Nilipokuwa mbunge wa Kawe barabara ya Chuo cha Ardhi, Makongo Juu na Goba ilikuwa na changamoto kubwa sana, tukafanikiwa kujenga kipande cha Goba mpaka Makongo Juu, 2020 kipande cha Makongo Juu hadi Chuo akapatikana mkandarasi ambaye angejenga ndani ya mwaka mmoja, mpaka sasa mkandarasi anasuasua, sasa nataka Waziri wa Ujenzi aniambie ni lini kipande cha barabara cha Makongo Juu kwenda Chuo cha Ardhi kitakamilika na kwa viwango vyote," ameuliza Halima Mdee





