Dkt. Mwele Ntuli Malecela enzi za uhai wake
Taarifa ya kifo cha Dkt. Mwele ambaye alizaliwa Machi 26, 1963, imethibitishwa leo Februari 10, 2022 na familia yake.
Mbali na nafasi ambayo amafariki akiitumia lakini amewahi pia kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya tafiti za kiafya Tanzania (NIMR).
Pia aliwahi kujihusisha na siasa ambapo mwaka 2015 aliwania nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa Uraisi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015.
Tangu Aprili 2017, Dkt. Mwele Malecela alikuwa akifanya kazi na Shirika la Afya Duniani (WHO) katika nafasi ya Mkurugenzi wa Udhibiti w a Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele.

