Eneo la ajali mlima Kitonga
Ajali hiyo imetokea mchana wa leo Jumapili, Februari 13, 2022. Majeruhi wanaendelea na matibabu kutoka kwa matabibu wa Mkoa wa Iringa.
Wafanyakazi hao walikuwa wanakwenda mkoani Mbeya kwa ajili ya kazi ya kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu ya NBC.
Uongozi wa Azam Media Limited umethitisha kutokea kwa ajali hiyo na umewashukuru wote waliotoa msaada wa hali na mali na kuwaomba Watanzania wote kuwaombea majeruhi nafuu ya mapema.

