(Nyota wa LA Lakers, Lebron James akifungwa kwa ku-dunk kwenye NBA)
Lebron amefikisha alama hizo alfajiri ya kuamkia Jumapili ya Februari 13, 2022 alipofunga alama 26 kwenye mchezo wa Ligi hiyo dhidi ya Golden State Warriors mchezo ambao Lakers walifungwa kwa alama 117-115.
Rekodi hiyo imezua mjadala baada ya nyota huyo mwenye miaka 37, imeibua mjadala mkubwa kwa wapenzi wa mchezo huo kujadili kati yake na Kobe Bryant ni nani mchezaji bora wa muda wote wa NBA kuwahi kutokea!
Mjadala huo unazidi kuwa gumzo baada nyota huyo kuvunja na kuweka rekodi nyingi ambazo hata Gwiji wa zamani wa Lakers marehemu Kobe Bryant hakuwa ameziweka ikiwemo hii ya ufungaji bora wa muda wote.

