Monday , 14th Feb , 2022

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ameiongoza timu yake kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Norwich kwenye EPL Jumamosi Februari 12, 2022 na kuweka rekodi ya kufikisha ushindi wake wa 550.

(Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola)

Ushindi wa michezo hiyo ya Pep imekuja baada ya kuongoza vilabu vya Barcelona, Bayern Munich na Manchester City kwenye michezo 738, akitoa sare michezo 97, kufungwa michezo 91 na kubeba mataji 33.

Pep aliiongoza Barcelona kushinda michezo 179, Bayern Munich michezo 124 na Manchester City kushinda michezo 247 hivyo kutimiza ushindi katika michezo 550 kati ya 738 aliyoviongoza vilabu hivyo vikubwa Duniani.

Ushindi huo pia umewafanya Manchester City kufikisha alama 63 wakiwa na michezo 25 na kuendelea kuwa vinara wa Ligi kuu ya ‘EPL’ kwa utofauti wa alama 9 na Majogoo wa Jiji , Liverpool wenye alama 54 na mchezo mkononi.