Nahodha wa Manchester United Harry Maguire
Harry Maguire amekuwa akicheza chini yakiwango na amekuwa na makosa mengi binafsi ambayo yamekuwa yakipelekea Manchester United kufungwa au kupata sare kwenye michezo ambayo walikuwa kwenye nafasi ya kushinda, kwa siku za karibuni beki huyo raia wa Englanda alifanya makosa ambayo yalisababisha kufungwa goli kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Burnley na wakapoteza kwa bao 1-0.
Kuhusu Maguire kocha Rangnick amesema “Kwenye michezo miwili ilyopita, ndio alionyesha madhaifu kwenye matukio kadhaa dhidi ya Southampton na goli tulilofungwa na Burnley. Lakini huyu ni nahodha wetu na sioni sababu ya kufanya mabadiliko”.
Kwa upande mwingine kuelekea mchezo wa usiku wa leo utakaochezwa katika dimba la OLD Traford, kiungo Fred atakuwa akirejea baada ya kupona alikosa michezo kadhaa kutokana na kukutwa na maambukizi ya uviko 19 lakini Ednson Cavan na Nemanja Matic wanamajeruhi hivyo hawatakwa sehemu ya mchezo huu.
Kwa wapinzani wao Brighton kocha Graham Potter hana majeruhi kwenye kikosi chake kile kilichocheza mchezo wa Ligi Kuu uliopita dhidi ya Watford ambao walishinda kwa mbao 2-0. Rekodi pia zinaibeba Manchester United kwani kwenye michezo 5 iliyopita dhidi ya Brighton wameshinda yote na katika michezo 13 kwenye michuano yote waliocheza OLD Traford Manchester wameshinda 11 na sare 2.





