Wachezaji wa Simba na Yanga wakiwania mpira kwenye moja ya michezo ya Ligi Kuu
Baada ya droo hiyo kufanyika mabingwa watetezi Simba SC wamepangwa kucheza na Pamba FC ya Mwanza Pamba ikiwa ndio timu pekee ya Championship iliyosalia kwenye michuano hii, Yanga SC wataminyana na Geita Gold ya Mkoani Geita, Azam FC wataminyana na Polisi Tanzania na wagosi wakaa Makumgushi Coastal Union wao watakipiga dhidi ya Kagera Sugara.
Katika hatua ya nusu fainali mshindi wa mchezo wa Yanga dhidi ya Geita Gold atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Pamba FC, na mshindi wa mchezo kati ya Azam FC na Polisi Tanzania atacheza na mshindi wa mchezo wa Coastal Unioni na Kagera Sugar.
Michezo ya hatua ya robo fainali itachezwa kati ya Aprili 8 mpaka 13, na hatua ya nusu fainali itachezwa katikati ya mwezi Mei, huku fainali ikitarajiwa kufanyika baada ya msimu wa Ligi Kuu NBC Premier League kumalizika.





