(Kocha msaidi wa Simba Suleiman Matola)

(Wachezaji wa Simba wakiwa mazoezini Morocco)
Matola alisema sababu ya kubaki Casablanca ni ili wafanye mazoezi yakutosha na kujiweka sawa sababu hawakupata muda wakufanya mazoezi tangu jumatatu walipo ondoka nchini Niger kwenda Uturuki, hivyo baada mazoezi hayo ya siku mbili katika jiji la Casablanca, kesho ijumaa ndio wanatarajia kufanya safari kuelekea mjini Berkane kwa ajili ya mchezo wao wa jumapili dhidi ya wenyeji wao RS Berkane, ambao ni mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Africa.
Pia kocha Matola amesema kiungo Jonas Mkude aliyeugua wakiwa safarini nchini Niger sasa yuko vizuri na ameshiriki mazoezi pamoja na timu siku ya jana hivyo anaweza kua sehemu ya mchezo wa jumapili. Vile vile Matola amewashukuru sana klabu ya Wydad casablanca kwa mapokezi mazuri waliowapa hadi kuwapelekea basi la kuwapokea uwanja wa ndege na kuwapeleka walipofikia.
Simba ndio wanaongoza kundi D wakiwa na alama 4 mbele ya RS Berkane mwenye alama 3, akifuatia na Asec Mimosas mwenye alama 3 pia, huku Union Sportive Gendermarine nationale akiburuza mkia akiwa na alama 1.


