Thursday , 24th Feb , 2022

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, ametoa hotuba fupi kwa taifa na kutangaza kwa sheria za jeshi zitaanza kutumika nchi nzima na kuwataka wananchi wake kutokuwa na hofu na wapo tayari kwa kila kitu na ushindi upo juu yao licha ya Urusi kushambulia miundombinu ya kijeshi ya nchi hiyo.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy

Jeshi la Urusi limeshambulia miundombinu ya kijeshi ya Ukraine pamoja na kujeruhi baadhi ya wanajeshi waliopo mpakani, huku matumaini makubwa pia wakiyapata baada ya Rais wa Marekani Joe Biden, kuahidi kushirikiana na Ukraine katika vuguvugu hilo dhidi ya Urusi.

"Kuanzia leo naomba mtulie majumbani, jeshi lipo kazini pamoja na vyombo vyote vya ulinzi," amesema Rais Zelenskyy.

Aidha, kwa hali inayoendelea nchini Ukraine hivi sasa watu wengi wanaukimbia mji mkuu wa Kyiv na wengine wanakimbia katika vituo vya treni chini ya ardhi ili kupata makazi.