(Kombe la FA nchini England)
Na klabu ya Southampton wao watakuwa wenyeji wa matajiri wa jiji la manchester Manchester City, huku Liverpool wakisubiri kucheza na mshindi kati ya Nottingham Forest na Huddersfield Town, ambazo zitacheza mchezo wao wa raundi ya tano siku ya Jumatatu machi 7, na timu hizi mbili ndio ziliwatoa mabingwa wawili wa hivi karibuni wa Kombe la FA, Leicester City pamoja na Arsenal.
Na Crystal Palace itacheza na Everton baada ya vijana hao wa Frank Lampard kuwachapa Boreham Wood bao 2- 0 usiku wa kuamkia leo, mabao yaliyofungwa na Salomon Rondon.
Namichezo hiyo ya hatua ya robo fainali ya kombe la FA inatarajiwa kuchezwa kati ya Ijumaa ya Machi 18 na Jumatatu ya Machi 21 mwak ahuu 2022.





