Sunday , 6th Mar , 2022

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe, ameomba aruhusiwe kuendelea kunyamaza kwa kipindi hiki ili awaone ndugu na familia yake pamoja na wakristo wenzake na wakati wa kuzungumza utakapofika atazungumza na Taifa.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Machi 6, 2022, wakati aliposhiriki ibada na kutoa shukrani katika kanisa la KKT Azania Front, Posta Dar es Salaam.

"Nilivyotoka gerezani waandishi wa habari walikua wakinitaka nizungumze na nilikua na nia dhahiri ya kuzungumza na Taifa lakini niliwaomba radhi nikawaambia kitabu chetu cha Mhubiri sura ya 3 kinasema kila jambo chini ya Mbingu lina wakati wake kuna wakati wa kusema na wakati wa kunyamaza, niruhusini ninyamaze niwaone familia yangu, ndugu zangu na wakristo wenzangu, utafika muda nitazungumza na Taifa,'' amesema Mbowe