Wednesday , 9th Mar , 2022

Mabingwa wa kihistoria wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, Real Madrid itawakosa nyota wake kiungo Casemiro na beki wa kushoto Ferland Mendy kwenye mchezo wa 16 bora wa michuano hiyo dhidi ya PSG ya Ufaransa utakaochezwa saa 5:00 usiku wa leo.

(Ferland Mendy na Casemiro wa Real Madrid)

Nyota hao watakosekana kutokana na kuoneshwa kadi mbili za njano hivyo kutumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja huku kiungo mkabaji Federico Valverde na beki wa kushoto Mkongwe Marcelo wakitazamiwa kuchukua nafasi zao

Real Madrid ina kibarua kigumu cha kupindua meza kwani walifungwa bao moja kwa sifuri kwenye mchezo wao wa mkondo wa kwanza nchini Ufaransa kwa bao la Kylian Mbappe ambapo inaelezwa huenda akawafiti kucheza mchezo huo.

Naye matajiri wa jiji la Manchester, Manchester City watakuwa wenyeji wa Sporting Lisbon ya Ureno huku akiwa na faida ya ushindi wa mabao 5-0 kwenye mchezo wao wa mkondo wa kwanza.