kikosi cha klabu ya Simba Sc
Meneja wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amesema wameingia mapema kambini kwa ajili ya kuonesha umuhimu wa mchezo huo huku nyota wawili pekee ambao watakosekana kwenye mchezo huo.
"Taarifa ya awali kuhusu majeruhi ni kuwa Hassan Dilunga atakosekana kwenye mchezo na Clotas Chama anakosekana kutokana na kanuni za kimashindano ila Taddeo Lwanga, Kibu Denis, Chris Mugalu na Jonas Mkude wapo tayari kwa mchezo. Berkane wamekuja wakati mbaya maana wametukuta tuko kamili."- amesema Ahmed Ally.
Klabu ya Rs Berkane ambayo ni kinara wa kundi D inatarajiwa kuwasili kesho majira ya saa sita kamili mchana huku Simba ikikamata nafasi ya pili wakiwa na alama 4 sawa na timu ya US Gendermarie ya Niger huku Asec Mimosa ya Ivory Coast wakiwa wa mwisho na alama 3.






.jpeg?itok=uqe_Ivr6)