Kocha Ralph Hasenhuttl
Alipo ulizwa kuhusu kuhusishwa na kibarua cha kuwa kocha mkuu wa Manchester united kocha huyo alisisitiza kuwa ukiona hivyo basi kuna kazi nzuri inafanyika lakini hana muda wa kufuatilia taarifa hizo,
"Nikiwa najadil kwenye kila orodha ambayo nimekuwa nikitajwa katika miezi miwili iliyopita, ni singekuwa na wakati wa kufanya kazi au kufanya kazi yangu. Kitu pekee ninachoweza kusema ni inaonyesha kwamba hatufanyi kazi mbaya hapa (Southampton).'' Amesema Hasenhuttl
Ralph Hasenhuttl raia wa Austria amekiongoza vyema kikosi cha watakatifu kutoka pwani ya kusini ya England ambapo kwa sasa kikosi hicho kipo nafasi ya 9 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England EPL wakiwa na alama 35. Huku akiwa hajafungwa na timu zote za Jiji la Manchester, Manchester United na Manchester City aketoka sare kwenye michezo yote ya Ligi Kuu.
Hasenhuttl anahusisha na Manchester United kutoka na mahusiano ya karibu na kocha wa muda wa sasa wa kikosi hicho Ralf Rangnick ambaye mwishoni mwa msimu huu, atachukua majukumu mapya ya kuwa mshauri wa ufundi wa klabu hiyo na yeye ndioe atakayeshauri ni kocha gani atafaa kukiongoza kikosi hicho kuanzia msimu ujao.
Wawili hawa walifanya kazi pamoja katika klabu ya RB Leipzing ya Ujerumani Husenhuttl alikuwa kocha mkuu na Rangnick alikuwa mkurugenzi wa michezo hivyo wawili hawa wanajua vyema.
Kocha wa PSG ya Ufaransa Mauricio Pochettino na Eric Ten Hag ndio wanatajwa kuwa ni machaguo ya kwanza kwa kikosi hicho cha mashetani wekundu na endapo kama itashindikana basi huwenda wakaamua kufanya Mazungumzo na kocha wa timu ya taifa ya Hispania Luis Enrique na kocha wa sasa wa Real Madrid Carlo Ancelloti.






