(Nyota wa tennis Novak Djokovic)
Djokovic mwenye umri wa miaka 34 ambaye ni mshindi wa mara 20 wa taji la Grandslam ameshindwa kukidhi vigezo vya ushiriki ambacho kinataka mshiriki kuwa amepata chanjo ya Uviko 19 kwa washiriki ambao sio raia wa Marekani.
"niombe radhi kwa mashabiki wangu kwamba sitashiriki kwenye michuano ya Indian Wells,sehemu nzuri nipapendapo kucheza na natumaini tutaonana tena mwakani"ameandika Djokovic kwenye mtandao wake wa twitter
Matumaini ya Novak Djokovic yalikuwa kupewa kibali maalumu kutoka idara ya afya ya Marekani CDC ambayo imekataa kulegeza masharti huku nafasi yake ikichukuliwa na nyota kutoka Bulgaria Grigor Dimitrov ilhali kwa Joker hili litakuwa shindano la pili kukosa kushiriki baada ya Australian Open 2022.






