
Trevor Noah alitoa maoni yake kupitia cha "The Daily Show".
"Mambo anayopitia Kim yanatisha kutazama, na hii inatupa mwanga wa kuona mambo mengi wanayopitia wanawake pale wanapojaribu kutoka katika ndoa. Hii tunaona kwa mwanamke mwenye nguvu Duniani, tajiri na maarufu anavyopata ugumu wa kumzuia mtu aliyeachana nae aache kumtafuta, kumfuatilia na kumnyanyasa.'' amesema Trevor Noah.
Baada ya kauli hiyo ya Trevor Noah kupitia kipindi cha "The Daily Show", Kanye West amepost picha za wachekeshaji anaowakubali kupitia instagram na kumdhihaki Trevor Noah na mashairi ya wimbo wa "Kumbaya, My Lord''.