
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha
Msitha ametoa rai wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa mafunzo hayo katika moja ya kumbi za uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuwekeza katika michezo hivyo ni vyema kukawa na wataalamu wengi zaidi katika michezo mbalimbali kwa maendeleo ya michezo nchini.
“kwanza naomba tuyape uzito mafunzo tunayopata hapa,najuwa wengi wetu tumeacha vitu vingi vya kufanya na kuja kuhudhuria mafunzo haya ili kupata ujuzi na tuweze kuendeleza mchezo wa riadha nchini,na hili tutaliweza pale tu tutakapoamua kulipa suala hili uzito, kufuatilia na kuzingatia ndani ya hizi siku tano (5) tulizonazo hapa,kuhakikisha kwamba tunachofundishwa tunakizingatia na kukifanyia kazi, niwakumbushe tu kwamba Serikali yetu ya awamu ya Sita (6) inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, tunafarijika sana imedhamiria kuwekeza katika michezo hivyo ni vyema tukiongeza wataalamu zaidi ili na sisi tuweze kutoa watu nje kwenda kufundisha michezo mbalimbali jambo ambalo litazidisha kasi ya maendeleo ya michezo yetu nchini,”amesema Msitha
Aidha Msitha amesema pia kupitia mafunzo mbalimbali ambayo Serikali inaandaa kwa kushirikiana na vyama vya michezo vya kitaifa, Tanzania itakuwa na wataalamu wengi zaidi wenye weledi katika michezo na kuacha kutegemea wataalamu kutoka nje ya nchi kama vile makocha na wengineo.
“kupitia mafunzo haya na mengine mengi yatakayofanyika, nchi yetu itakuwa na wataalamu wengi wenye weledi, hatuna sababu tena ya kuendelea kutegemea makocha kutoka nchi za jirani,kwa hiyo tujipange kwa hii fursa ndogo tuliyoipata tuitumie vizuri ipasavyo,”amesema Msitha