
Mama mzazi wa kijana anasema sasa wanalazimika kumfungia ndani kijana huyo kwa kuhofia kutendewa tena tukio hilo.
EATV imefika nyumbani kwa wazazi wa kijana huyo eneo la manzese na kuzungumza na majeruhi ambae anasema walikuwa na rafiki yake lakini walimchukua yeye na kuanza kufanya jitihada za kukata mkono wake lakini kelele zilisaidia watu kujitokeza na wahusika kutokomea.
Mariam Kessy ambaye ni mama mzazi wa kijana huyo anasema tukio hili ni mara ya pili kumtokea kijana huyo ambapo mara ya kwanza lilimtokea shuleni ambapo mtu alijaribu kuingia lakini ulinzi ukawa mzuri akashindwa kutekeleza uhalifu huo.
Mama huyo amasema kwa sasa anahofia hata kumruhusu kijana wake kutoka nje na kutembea mtaani kutokana na kuhofia kutendeka tena kwa uhalifu huo.
Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mferejini na Mwakilishi wa mwenyekiti Hamis Yusuph anasema Uongozi wa serikali ya mtaa Mferejini wanaendelea na uchunguzi kufahamu wahusika hao kwa kuwa ni tukio la kwanza la aina hiyo kutokea katika eneo lao
Mussa Kabimba ambaye ni Katibu mkuu chama cha wenye ualibino Tanzania (TAS) amewataka watanzania kuendelea kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama kuhusu matukio ya aina hiyo