Friday , 29th Apr , 2022

Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, amesema kwamba umaskini hauwezi kufutika nchini endapo uchumi hautapanda kwa asilimia 8  na kuendelea.

Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo

Kauli hiyo ameitoa hii leo Aprili 29, 2022, Bungeni Dodoma, wakati akichangia kwenye Bunge la bajeti.

"Ndugu zangu Watanzania uchumi usipokuwa kwa kadri ya kiwango cha asilimia 8, 10 na kuendelea, hatuwezi kuufuta umaskini nchini hapa, kitu kitakachotusaidia ni kwenye sekta za uzalishaji muhimu ambazo ni kilimo, ufugaji na uvuvi na kingine ni lazima twende kwenye uchumi wa gesi," amesema Profesa Muhongo