Sunday , 1st May , 2022

Mtoto mchanga aliyeachwa na marehemu Mbunge wa viti maalum mkoa wa Rukwa Irene Ndyamkama, amefariki dunia jana Aprili 30, 2022,  baada ya kuishi kwa siku saba. 

Marehemu Irene Ndyamkama

Mbunge Irene alifariki dunia Aprili 24, 2022, katika hospitali ya Tumbi wakati akipatiwa matibabu na alizikwa Aprili 29 mwaka huu kijijini kwa mama yake Isinde, Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi.