Tuesday , 3rd May , 2022

Vikosi vya kiusalama Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, vimemuua kwa kumpiga risasi tano mnyama aina ya Fisi, aliyemvamia na kumjeruhi mtoto mdogo Gindu Kilulu, mkazi wa Mtaa wa Yoma Kata ya Somanda wilayani humo.

Mtoto mdogo, Gindu Kilulu mwenye umri wa miaka 6 aliyekuwa amembeba pia mtoto mwenzake mgongoni, amenusurika kuuawa na fisi baada ya kumvamia saa 2 asubuhi wakati akimpeleka mtoto mwenzake huyo kwa mama yake aliyekuwa akikamua maziwa.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Lupakisyo Andrea Mjukuu wa Kapange, amesema Serikali haitambakisha fisi yoyote atakayetokea kushambulia binadamu.