Wednesday , 4th May , 2022

Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima, ametoa pole ya shilingi laki moja kwa kila mwananchi aliyejatwa mapanga katika mtaa wa Mtongani Kunduchi usiku wa kuamkia Mei 2, 2022. 

Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima, akitoa pesa kwa wananchi waliojeruhiwa na Panya road

Kiasi hicho cha pesa amekitoa leo Mei 4, 2022, baada ya mbunge huyo pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, kwenda kuwatembelea na kuwajulia hali waliojeruhiwa na vijana hao.

Jumla ya wananchi 19 katika mtaa huo walijeruhiwa kwa mapanga na vijana wanaodaiwa kuwa ni Panya road usiku wa kuamkia Mei 2, 2022.