
Kocha Mkuu wa Simba Pablo Franco
Pablo amesema wao kama timu kubwa inayopambania ubingwa hawatakiwi kufanya makosa kama yale ambayo yanazidi kuwaweka katika mazingira magumu.
Mbali na safu ya ulinzi kufanya makosa Pablo amesema pia hakuwa vizuri katika kumalizia nafasi tuwalizopata hasa kipindi cha kwanza.
“Kwa timu kubwa kufanya makosa ya kiulinzi kama vile haileti picha nzuri. Pia tumetengeneza nafasi ambazo hatukuzitumia vizuri.
“Tutarudi kuendelea kujipanga kwa mchezo unaofuata, bado hatujakata tamaa tutahakikisha tunapambana kupata alama tatu kwenye kila mechi,” amesema Pablo.