Thursday , 5th May , 2022

Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah amewapa ujumbe wachezaji wenzake kwamba lazime waifunge klabu ya Real Madrid kwenye mchezo wa fainali wa Uefa champions league utakaofanyika jijini Paris mnamo 28,2022.

(Nyota wa Liverpool Mohamed Salah)

Real Madrid imewaondosha klabu ya Manchester City kwa jumla ya magoli 6-5 kwenye hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya (Uefa champions league ) baada  ya kuchomoza na ushindi wa magoli 3-1 kwenye dimba la Santiago Bernabeu,nchini Hispania.

"tulipoteza kwenye mchezo wa fainali dhidi yao,nataka kucheza na wao na matumaini yangu tutapata ushindi na sisi kwenye mchezo huo “amesema Salah ambaye kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Madrid mara ya mwisho alishindwa kumaliza mchezo kutokana na kuumizwa bega na mlinzi Sergio Ramos kwenye mchezo huo.

Madrid watakutana na Liverpool kwenye mchezo wa fainali utakaochezwa mnamo May 28,2022 huku mara ya mwisho kwa miamba hiyo kukutana ilikuwa msimu wa 2017/18 ambapo Madrid walichomoza na ushindi wa magoli 3 kwa 1 kwenye uwanja wa NSC Olimpiysky mjini Kyiv nchini Ukraine