
Makamu Mwenyekiti (CHANETA), Shyrose Bhanji .
Rai hiyo imetolewa leo Mei 05, 2022 na Afisa michezo mkuu wa Baraza la Michezo Taifa na Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi mdogo wa chama hicho Allen Alex, uchaguzi wa kujaza nafasi zilizokuwa wazi baada ya kukamilika kwa uchaguzi Mkuu ulifanyika Octoba 2021 Jijini Dodoma.
"Watu ni Soko na soko ndilo litasaidia kuwavutia wadhamini na kuufanya mchezo ukue, hawa wamerudi kuvunja rekodi yao, hivyo wasukumeni wafanye kile mnachotaka wakatekeleze yale mnayokusudia kuirudisha hadhi ya netiboli,"alisema Mwenyekiti wa Uchaguzi na kuongoza kuwa;
"Dunia imekua shirikisheni watoto wa kike itakuwa kivutio katika kutangaza mchezo kupitia mitandao yao ya kijamii ili dunia itambue uwepo wenu,"alisisitiza.
Matokeo ya uchaguzi huo nafasi ya Makamu Mwenyekiti Shy Rose Banji ameibuka kidedea kwa kupata kura zote 34 baada ya kumshinda mpinzani wake Dkt Juliana Manyerere ambaye ameambulia patupu.
Wakati Rose Mkisi akiwabwaga wapinzani wake watatu kwa kupata kura 19 katika nafasi ya Katibu Mkuu ambao ni Jaqline Sikozi aliyepata kura nane, Rahma Kilimba kura saba na Damiani Chonya ambaye hakupata kura.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Shyrose Bhanji amesema wanaandaa mipango kabambe kurejesha hadhi ya mchezo huo nchini hasa katika ushindani katika anga za kimataifa.
Shy -rose alisema watashirikiana na viongozi wenzake kuhakikisha wanashiriki mashindano ya Kimataifa yakiwamo Afrika Mashariki na Kati, Afrika na Kombe la Dunia.
"Tumerejea katika mchezo tunaoufahamu na kazi yetu ni kupanga mipango itakayowavutia wadau, tutashirikiana katika kurudisha hadhi na heshima ya mchezo huu kama awali," amesema Shy-rose.