
Mwanasiasa huyo anasema zao la bangi lina uwezo wa kufufua uchumi wa nchi hiyo na hata kulipa deni la nchi hiyo linalodaiwa na mataifa mbalimbali.
Pamoja na kuhalalisha bangi mwanasiasa huyo ameahidi kuwa atateua Mawaziri Wakuu wanane, kusitisha katiba kwa miezi sita na kazi nchini humo zitafanywa kwa siku nne pekee kwa wiki.
Sera hizo amezitoa wakati akimtangaza Justina Wambui Wamae kama mgombea mwenza na kumfanya mgombea mwenza wa kwanza wa kike katika historia ya Kenya.