Monday , 16th May , 2022

Michezo ya nusu fainali ya kanda ya Mashariki na magharibi ya ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA imekamilika usiku wa kuamkia leo na kushuhudia timu za Boston Celtics na Dallas Mavericks zikifuzu hatua ya fainali.

Wachezaji wa Boston Celtics wakishangilia kwenye mchezo dhidi ya Bucks

Boston Celtics imefuzu fainali ya ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA ukanda wa Mashariki baada ya kushinda mchezo wa 4 katika mfululizona wa michezo 7 ya nusu fainali kwa kuifunga Milwaukee Bucks na kuwavua ubingwa wa NBA kwa alama 109 kwa 81.

Katika mchezo huu Grant Williams wa Boston Celtics amefunga alama 27 rebound 6. Na katika mchezo wa fainali Celtics watacheza dhidi ya Miami Heat. Na nyota wa Backs Giannis Antetokounmpo amefunga alama 25, pasi za kufunga (assists) 9 na rebound 20 lakini haikutosha kuwafanya mabingwa hawa wa msimu uliopita kusonga mbele.

Ukanda wa Magharibi Dallas Mavericks nao wamefuzu Fainali baada ya kushinda mchezo wa 7 kwa kuifunga Phoenix Suns kwa alama 123 kwa 90.

Mchezaji nyota wa Dallas Luka Doncic amefunga alama 35, pasi za kufunga (Assists) 4 na Rebound 10. Katika hatua ya fainali Mavericks watacheza dhidi ya Golden State Warriors.