Mizinga ya Nyuki
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa uendelezaji ufugaji Nyuki Daniel Charles Pancras, amesema hayo wakati wa zoezi la uwekaji wa mizinga ya Nyuki zaidi ya elfu ishirini na saba na mia sita katika pori la Manga, ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa maadhishi ya siku ya Nyuki ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Katavi.
"Mizinga ya jadi ambayo wazee wetu wanatumia sio mibaya na inazalisha asali lakini asali yake inatoka sio nzuri ,sasa tunahamasisha tutoke kwenye mizinga ya jadi twende kwenye mizinga ya kisasa ambayo inasaidia asali kutoka nzuri na inakuwa haina maji," amesema Mkurugenzi msaidizi wa uendelezaji wa ufugaji Nyuki
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa, Mwanamvua Mrindoko, amewataka wananchi kutunza misitu ili waweze kupata maeneo ya kufugia Nyuki na wavune asali kwa wingi.