Monday , 23rd May , 2022

Katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka amesema juhudi zinazofanywa na Mwenyekiti wa Chama hicho Rais Samia Suluhu Hassan kuzungumza na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa inaonyesha jinsi gani alivyorejesha heshima ya Demokrasia

Katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka

Akizungumza kwenye ofisi kuu ya CCM Dodoma amesema kuwa hiyo ni moja ya njia ya Watanzania kulinda tunu ya Taifa na uwepo wa Demokrasia endelevu nchini ili kuweza kuijenga Nchi. 

Shaka amewahakikishia Watanzania kuendelea kunufaika katika uimarishwaji wa misingi ya haki utawala bora na utoaji huduma za kijamii, kiuchumi na kisiasa.